Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema hatajiuzulu kutokana na hoja ya kumwondoa madarakani kwani hajafanya kitu chochote kwa Wakenya, hivyo atapigania haki yake kubakia katika nafasi hiyo. Bunge la Kenya leo linatarajia kujadili hoja ya kumwondoa ofisini ambapo Gachagua ameapa kufika bungeni ili kupinga madai 11 dhidi yake yaliyowasilishwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse mwezi Septemba. Naibu Rais, Rigathi Gachagua anatarajiwa kufika mbele ya Bunge la Kitaifa kwaajili ya kutetea nafasi yake (Unaibu Rais) dhidi ya hoja za kumwondoa Madarakani zilizowasilishwa na Septemba 26, 2024 na Mbunge wa Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse. Hatua hiyo inafuatia mchakato wa...